Breaking News

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2013

Nawatakia heri na fanaka ya mwaka mpya mwaka 2013 huwe wenye mafanikio kwenu, lakini mafanikio yoyote yale hayaji bila uthubutu. Lazima watu tuwe na hali ya kuthubutu ili tuweze kufika pale tunapohitaji kufika.
Binadamu wa leo wameshindwa kuwa na uthubutu wakidhani watachekwa na wenzao endapo watakosea mahala fulani, kitendo ambacho kinawakwamisha kufikia pale wanapohitaji kufika. Uthubutu ni nyenzo muhimu katika mafanikio yako, kama wewe ni mwanafunzi, mfanyabiashara, mwalimu, mwanasiasa au mtu yoyote yule jenga tabia ya kuthubutu kufanya kile kilicho bola kwako. Kwa mfano watu wenye elimu hivi sasa elimu yao ndio imekuwa kikwazo cha maendeleo yao, kwa sababu wanakuwa "very selective" katika kila jambo. Wanataka kuwa na kazi nzuri kutokana na elimu waliokuwanayo, lakini kama kuna kazi yenye pesa na yakudharaulika. Mtu mwenye elimu anashindwa kufanya kazi hiyo akiona kuwa watu watamfikiriaje na elimu aliyokuwanayo. Kwa hiyo mtu kama huyu amekosa uthubutu. 

Vilevile ata kwa mwanafunzi ni vizuri kuwa na uthubutu katika masomo yako, maana hakuna somo lililo gumu na hakuna somo lililo jepesi. Masomo yote yapo sawa na ndio maana katika kila somo wapo wanaopasi vilevile wapo wanaoanguka. Kwa hiyo wale wanaopasi siku zote wanakuwa na uthubutu wa kujituma kwa bidii bila kujali kuwa wataonekana wamekosea. Pia wale wanaoanguka wamekosa uthubutu sababu unapothubutu ndipo unapotambua udhaifu wako au makosa yako yapo wapi. Tujenge tabia ya kuthubutu ila tuthubutu kwa kile kilicho bora. If you don't want to dare, how you are going to achieve something special?! Once again nawatakia heri na fanaka ya mwaka mpya 2013.