Breaking News

NDOTO YASABABISHA KIFO KWA MTU MMOJA ALIEKUWA KWENYE TRAINI KUTOKEA MPANDA KUELEKEA DAR

Hapa askari wakiuchukua mwili wa marehemu huyo leo asubuhi ambapo traini ilipowasili mjini Dodoma. Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu alikuwa anatokea Mpanda kuelekea pwani, vituo viwili kabla ya kuingia Dodoma abiria wenzake waliokuwanae karibu wakatangaza mwenzao kajirusha kupitia dirishani baada ya kukurupuka kutoka usingizini. Inaonekana kuwa marehemu alipokuwa amelala alikuwa anaota ndoto mbaya ambayo ilimshitua na kumfanya ajirushe nje ya traini wakati ipo katika mwendo kasi. Kitendo icho kilipelekea kupoteza uhai kwa mtu huyo baada kupasuka kichwa.

Hapa mwili wa marehemu huyo umeishawekwa kwenye gari la polisi ili kwenda kuifadhiwa sehemu husika


Hapa mwili wa marehemu ulikuwa umeifadhiwa kwenye breki yaani behewa la mwisho la traini. Ambapo traini ilipoingia mjini Dodoma asubuhi ya leo mwili huo wa marehemu ulichukuliwa na jeshi la polisi kwenda kuifadhiwa sehemu husika.

Hapa abiria wakishangaa tukio ilo, niseme kwamba kifo hutokea wakati wowote na sehemu yoyote ile, sisi wote ni wake Mola na kwake tutajongea. Huwezi jua utakufa vipi ila cha muhimu tambua kuwa ipo siku utakufa, cha muhimu yatupasa tujiandae vyema na safari yetu ya mwisho.

Katika harakati zangu za hapa na pale niliweza kuongea na abiria mmoja, ambaye naye alikuwepo kwenye traini hiyo. Alisema kuwa " Tuliambia kuna mtu amejirusha nje wakati traini ikiwa katika mwendo kasi, hivyo traini ililazimika kusimama na kukata kichwa kurudi kumtafuta mtu huyo, ambapo baada ya masaa matatu walifanikiwa kumpata mtu huyo lakini kwa bahati mbaya alikuwa tayali kaishapoteza maisha, jamaa hakuwa na upungufu wa akili ila alikuwa amelala na baadae akashituka na kujirusha nje ya traini. Hivyo inawezekana alikuwa anaota ndoto mbaya".