Breaking News

Yangu Ya Moyoni











Ni wazi kwamba kwa namna moja au nyingine wanafunzi wa vyuo wanahali ngumu. Hii ni kutokana na walio wengi kutoka katika familia za kimasikini. Kitendo ambacho kinamfanya mwanafunzi kuchukua uamuzi wa kugoma pindi anapocheleweshewa kile kinachoitwa BOOM. Bila kujua matokeo ya mgomo yatakuwa na madhara gani kwake, na hii ni kwa sababu wanafunzi wanasahau maisha ya wazazi wao yapo vipi. Maana kuna wazazi wengine wanajinyima kwa hali na mali ili watoto wao waweze kusoma. Lakini wanafunzi wanajikuta wanagoma na hatimae wanasimamishwa masomo yao. Nayasema haya kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana kilichopo Dodoma maarufu kama St. John's University Of Tanzania. Nilikumbwa na madhara ya kusimamishwa masomo until further notice. Hii ilitokea kwa sababu wakati wanafunzi wenzangu wanagoma mimi nilikuwa nawapiga picha sababu napenda sana uandishi wa habari. Sikujua kama nitanukuliwa kama nimehusika na mgomo sababu nilikuwa mbali na wale wanaogoma. Lakini kile kinachoitwa screen kilinichukua na ikaonekana kama nami nimeshiriki katika mgomo huo. Ambapo baadae yalitolewa majina 15 ya wanafunzi ambao inasemekana ndio waliochochea mgomo huo, moja kati ya majina hayo lilikuwa lakwangu. Kwa hiyo mgomo vyuoni unaathiri wale waliogoma na wasiogoma kwa pamoja. Kwa sababu wanafunzi wote katika chuo chetu tulipewa masaa matatu ya kuhakikisha unafunga kilichokuwa chako na kwenda nyumbani. Na baadae unaporudi unatakiwa kusajiriwa upya ambapo zoezi ilo ni la siku mbili. Kushindwa kusajiliwa upya chuo kinakuwa hakikutambui kwa hiyo unakuwa umejifukuzisha mwenyewe. Napenda kuwaambia wanafunzi wenzangu kuwa "The hard way is the only way to survive" ni muhimu kuvumilia shida ya muda mchache ili uweze kuendelea na masomo yako kama kawaida. Yatupasa tuelewe kuwa PESA ni za kwetu na ipo siku tutapewa tu hata zichelewe vipi.