UNAFIKIRI NI NJIA IPI NZURI YA KUSHEREKEA MWAKA MPYA?
Kila mtu ananamna yake ya kusherekea mwaka mpya, utaona watu wengine wanatoka na madebe, makopo, ngoma pamoja na fimbo ya kupiga vitu hivyo ifikapo saa 6 kamili za usiku. Wengine ni chereko na mayowe na mtindo fulani wa mdundiko ambao watu watazunguuka mtaa kwa mtaa pale mwaka unapoingia. Mitaa ya uswahilini wanatabia ya kuchoma mataili ya magali ambayo yameishatumika, wakati mitaa ya uzunguni wanatabia ya kuchoma baruti ambazo zinakuwa zinarushwa angani na kusambaa au kuchanua kama maua. Watu wengine furaha zao zinapelekea kuvunja taa za majumba ya watu. Hii inatokea sababu mtu anashindwa fikiria ni namna ipi ambayo itakuwa bora katika kusherekea au kuukaribisha mwaka mpya. Ikiwa Mwenyezi Mungu amekuwezesha kukufikisha mwaka mwingine inapaswa kumshukuru kwa namna iliyo nzuri, maana kuna wengine walitamani kuuona mwaka mwingine lakini tumeishawazika na wametangulia mbele ya haki. Mtu mwenye busara siku zote hasherekei kwa kumbuguza mtu mwingine kwa namna moja au nyingine. Ikiwa unaelewa wewe ni msafiri basi ipo siku safari yako itawadia. Kwa hiyo unapaswa kujiuliza umefanya kipi ambacho ni chema katika mwaka uliokwisha au ulifanya kipi ambacho sio chema katika mwaka uliokwisha. Ukitambua haya basi utaupokea mwaka mpya kwa namna iliyo bora ambayo inampendeza Mungu wako. Ni watu wachache sana ambao wanafanya ibada katika kuupokea mwaka mpya, je wewe upaswi kufanya ibada? kwa kumshukuru mungu wako aliekuwezesha kukufanya kuwa mzima buheri wa afya njema. Sidhani kama Mungu anapendezwa kuona unamshukuru kwa kumpigia madebe, kuchoma mataili, kuvunja taa za watu. Yapasa ukae chini na ufikiri mara mbili.