Breaking News

Mrembo alietoka na CLARITHA aja tena na movie ya KIDUDUMTU.


Mrembo kutoka kampuni ya Makeke Modelling, anaejulikana kwa jina la Rachel B. Njingo ang'ara tena kwenye movie mpya inayokwenda kwa jina la KIDUDUMTU ambayo inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni. Hii itakuwa movie ya pili baada ya CLARITHA ambayo ilimtambulisha vizuri katika tasnia ya Bongo movie. Katika movie hii utapata kuwaona mastaa Adam Haji na Halima Yahaya walivyocheza kwa namna yao. Washiriki wengine ni Pierre Joseph, Jack Chars, Rashid Samuhura na Ahmed Makambaza.


Rachel B. Njingo akiongea na MWINYI BLOG amesema kuwa wapenzi wa Bongo Movie wajiandae kuiona movie mpya "Kidudumtu" inayotambulishwa na BlackHouse Media ambayo itakuwa na vionjo vya aina yake, ambapo kila muhusika amecheza vizuri katika nafasi yake. Hii si ya kuikosa pindi itokapo. Asante kwa kutembelea MWINYI BLOG naomba ubofye HAPA kuingia kwenye page yangu ya facebook na kulike page ili uendelee kupata burudani na matukio ya hapa na pale.