Breaking News

Dayna Nyange azungumzia ukimya wake


Dayna Nyange ni mmoja kati ya wasanii wachache sana wa kike wanaofanya vizuri katika mziki wa Bongo Flava. wimbo wa ‘Nivute Kwako’ ndio uliompa umaarufu mkubwa na akaweza kufanya show kibao akizunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Alitawala sana vyombo vya habari mwishoni mwa mwaka jana pale alipodai beat la wimbo wake kutumiwa na Diamond bila ya wao kuridhiana lakini mwisho wa siku kila mtu aliendelea na mambo yake.

Tangu sakata hilo la Dayna na Diamond kuisha, mwandada huyu amekua hasikiki sana katika masikio ya watu. Kwani hajatoa wimbo mpya kwa mda mrefu sasa. Dayna akihojiwa na tovuti ya BaabKubwa kuhusu ukimya wake katika game alisema “Siyo kama nipo kimya nimeishiwa hapana ila nilikuwa nina majukumu ya kifamilia kidogo, pamoja na kuendelea kusoma game coz kila siku muziki unakuwa na mashabiki wanahitaji vitu vipya kwa hiyo kama msanii hautakiwi kukurupuka katika kutoa wimbo. Nimefanya nyimbo nyingi ila kwa sasa naangalia ipi ianze so mashabiki wangu wakae tayari any days naachia jiwe jipya na siwezi kuwaangusha.” 
 
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.