Breaking News

Davido adai mkwanja mrefu, kupiga show nchini Kenya.


Haina ubishi kuwa Diamond Platnumz ndie msanii anayelipwa zaidi Tanzania, kwa hapa Bongo ili Diamond apige show lazima awe amelipwa mpunga sio chini ya millioni 10. Kwa Kenya anayeongoza ni Jaguar anayepokea zaidi ya milioni 15 za kibongo kwa kila show na Pia huwezi msahau Chameleone wa Uganda ambaye ili apige show lazima awe amelipwa zaidi ya milioni 8 za kibongo.

Inaweza kukushangaza lakini ukweli nikwamba siku chache zilizopita Davido aliombwa akafanye show nchini Kenya na akaomba alipwe zaidi ya milioni 4 za Kenya ambazo ni zaidi ya milioni 75 za Tanzania. Pia aliomba mapromota hao wa Kenya wamlipie nauli ya ndege yeye na wenzake 6 daraja “business class” na pesa ya matumizi pale watapofika nchini Kenya. Kwa hiyo ukichukua milioni 4 za Kenya alizotaka alipwe ukichanganya na hela yake ya nauli na matumizi unapata kama milioni 6 za Kenya ambazo ni sawa na milioni 113 za Tanzania.

Inadaiwa kuwa msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi Afrika ni Fally Ipupa, inadaiwa Fally aliwahi kukubaliana na mapromota wa Kenya kufanya show lakini alipofika hotelini aligoma kukaa kwa kuwa hotel hiyo sio ya hadhi yake.

 Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.