Sean “Puffy” Combs a.k.a P.Diddy kutoa hotuba (Speech) katika Graduation ya Howard University
Sean “Puffy” Combs aka P.Diddy ambae hivi sasa ameamua kurudi kwenye jina lake la zamani la kisanii “Puff Daddy” ambae nae pia alisoma katika university hiyo, imetangazea rasmi kuwa Tarehe 10 ya mwezi ujao kwenye mahafali (Graduation) ya wanafunzi waliomaliza chuo cha Haward cha huko nchini Marekani. Diddy atatoa speech kama iliyo ada kwa shule za nchini humo kwa watu maarufu kama hao kuweza kushare “inspiration success stories” za maisha yao. Siku ya jana chuo hicho kilitangaza kua msanii P Diddy atakua mtu pekee atakayetoa hotuba kwa wahitimu katika chuo hicho. Pia katika siku hiyo chuo hiko kimetangaza kua kitamtunuku Diddy Degree ya Humanities (Doctoral Degree of Humanities).
Sababu kubwa ya Diddy kuchaguliwa kua mzungumzaji katika siku hiyo ni kwamba aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo hicho akaacha (Drop Out) na kwa sasa ana mafanikio makubwa kimuziki na kibiashara. Diddy alichaguliwa kujiunga na chuo cha Howard mwaka mwishoni mwaka 1990 akisomea Degree ya biasgara (BA: Business Administration)
Baada ya uongozi wa chuo hicho kumtangaza Diddy kama mtoa hotuba, asilimia kubwa ya wahitimu walipinga uamuzi huo kwa madai kuwa Diddy ni bad influence kwa wanafunzi kutokana na mafanikio yake, lakini uongozi wa chuo hicho umegoma kutengua maamuzi yao. Baadhi ya watu maarufu walioacha chuo (Drop Outs) na bado wakaalikwa kua wageni rasmi katika Graduation za vyuo vikubwa huko Marekani ni “Bill Gates” na marehemu “Steve Jobs”.
Diddy ambae mwaka jana alifubgua kituo chake cha tv kijulikanacho kama “RevoltTV” ambacho kinadeal na entertainment peke yake, msanii huyu ameweza kupata zaidi ya watu milioni 20 (20 Million Viewers) nchini marekani peke yake. Bila kusahau Bad Boyz Records yenye wasanii wakubwa sana kwenye entertainment indusrty ya dunia, Sean John Clothing ambayo inauza kama Tommy Hilfigger, Gucci na kama kampuni nyingine za nguo, kinywaji “Diddy’s Drink” na chain ya Restaurants ijulikanayo kama “Justin’s” ambayo ni jina la mtoto wake wa kiume.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale