Justin Bieber anusurika kurudishwa CANADA
January 23 mwaka huu nchini Marekani kulianzishwa kampeni ya watu wanaopinga matendo anayofanya msanii Justin Bieber na kusaini fomu maalumu katika website ya White House ili msanii huyo anyanganywe vibali vya kuishi nchini humo. Jumla ya wananchi wa nchini humo wapatao 273,968 walisaini form hiyo kuilaImisha serikali hiyo kumuondoa mwanamuziki huyo.
Watu hao walichukua uamuzi huo baada ya kuona kuwa tabia za Justin Bieber zitasababisha vijana wengi kuiga matendo yake na kudai kuwa mfano mbaya kwa jamii nzima kwa ujumla. Justin amekumbwa na mikasa mingi ikiwemo kukamatwa akiendesha Gari huku kalewa, kuendesha gari huku leseni yake ya kuendesha ikiwa imeisha muda wake wa matumizi, kukamatwa na madawa ya kulevya na vituko vingine vingi.
Serikali ya Marekani imejibu maombi ya raia hao kuwa hawawezi kumnyang’anya Justin vibali vya kuishi Marekani kwa sababu kama atashtakiwa kwa kuleta vurugu au kama atafungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio sheria inaweza kumuondolea vibali hivyo, kwa vile Justin hajafanya yote hayo basi yupo huru kuendelea kukaa nchin humo.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale