Breaking News

DOWNLOAD:- Bongolos Ft. Asteria - Wape (mp3)


https://mkito.com/song/16702?referrer=016b6967239a2452a94d6d6a4ebcad94ca604cc7

Bongolos ni kundi la wanamuziki wawili, Drew (Kiume) na Tamu (Kike), lenye makazi yake jijini Dar es Salaam, Tanzania. Bongolos ni kundi lililoundwa na mtayarishaji mkongwe wa muziki Afrika Mashariki P-Funk Majani ndani ya Bongo Records mwaka 2016. Jina Bongolos lilipatikana kutoka kwa mwanamuziki wa hip hop wa Marekani, Mims baada ya kuja kufanya kolabo nchini Tanzania chini ya Bongo Records. Drew wa Bongolos alikutana na mtayarishaji P-Funk Majani baada ya kuona ujumbe mfupi wa maneno kwenye mitandao ya kijamii kwamba mtayarishaji huyo alikuwa anatafuta wanamuziki chipukizi. Tamu wa Bongolos alikutana na mtayarishaji huyo baada ya kuunganishwa na rafiki yake. Bongolos wanafanya muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa kufoka na kuimba ambao pia unawezwa kuitwa Bongo Flava. Muziki wao umejawa na vionjo vya Kiafrika kwenye mirindimo yake. Bongolos wameachia ngoma yao ya kwanza iitwayo Wape. Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.

No comments