Breaking News

DOWNLOAD: Damian Soul Ft Vanessa Mdee - KAUMBA (New Song)



https://mkito.com/song/11915?referrer=3fa7ec18d94ba488dd2b1341ee51c27e888fb353


Msanii wa R&B na Soul nchini, Damian Soul ameachia wimbo mpya alioupa jina ‘Kaumba.’ Muimbaji huyo mahiri ameachia ngoma hiyo inayofuatia wimbo wake Tudumishe aliomshirikisha rapper anayeheshimika Tanzania, G-Nako. 

Kwenye Kaumba Damian amemshirikisha Vanessa Mdee na unazungumzia jinsi Damian anavyompata msichana ambaye Mungu kamuumba zaidi hata ya matamanio ya moyo wake. Na kama jina lake lilivyo, wimbo huu wenye ladha ya soul na vionjo vya asili unawapa nafasi Damian na Vanessa kuimba kwa kujibizana kuhusu wanavyopendana.

Wimbo huu umetayarishwa kwa ushirikiano wa Damian Soul na Sappy. Sappy anafahamika pia kwa kutayarisha ngoma zilizofanya vizuri ukiwemo XO wa Joh Makini.  Wimbo huu una vionjo vya Sindimba ukiwa na sauti tamu za gitaa zilizocharazwa na Damian Soul mwenyewe huku Sappy akimalizia vitu vingine.

Damian Soul pia anajulikana kwa nyimbo kama Nipenzi aliomshirikisha Joh Makini, Dua la Kuku na Hakuna Matata. Kaumba unakuwa wimbo wake wa sita na ambao bila shaka utaonesha upande wake mwingine zaidi ya alivyozoeleka katika soul – ladha aliyoitoa kwa baba yake na unakuwa wimbo wa kwanza kumshirikisha Vanessa Mdee. 


DOKEZO KWA WAHARIRI

Damian Soul ni muimbaji wa vionjo mnyanganyiko vya Kiafrika (Afro Fusion) aliyejulikana kwa kushiriki kwenye msimu wa tano wa shindano la  Tusker Project Fame na pia kushiriki kwenye shindano la  Maisha Superstar. Anajulikana pia kwa kushiriki kwenye Jahazi Jazz Festival 2015 visiwani  Zanzibar alikopanda jukwaa moja na wanamuziki nguli wa Afrika na washindi wa tuzo za Grammy.

Sappy ni mtayarishaji wa muziki wa Tanzania anayefanyia kazi zake nchini Kenya na ameshafanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki wakiwemo Prezzo, Nameless, Redsan, Nazizi, Ben Pol, King Kaka na wengine. Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.