Breaking News

Rachel Bithulo aja na "Dead Samson"


Mrembo anaekwenda kwa jina la Rachel Bithulo yupo mbioni kuja na filamu mpya inayokwenda kwa jina la "Dead Samson" ambayo amecheza na Ahmed Makambaza pamoja na Albert Thadei. Movie nyingine mpya yaitwa "Why me?" yupo Grace Mapunda, Jengua na Mandizzo. Zote hizi baada ya uchaguzi zitakuwa mtaani. Binti huyu mwenye miaka 25 alitambua kipaji chake cha kuigiza mwaka 2010 alipokuwa sekondari na 2015 alifanikiwa kurekodi movie yake ya kwanza.
 Yafuatayo ni baadhi ya mahojiano yaliyofanyika kati ya Mwinyi Blog na Rachel Bithulo:
Mwinyi Blog: Unaizungumziaje Bongo movie ikiwa ndio kwanza umeingia katika tasnia hiyo?
Rachel Bithulo: Bongo movie wengi hufanya kazi kwa mazoea pia kujuana kwingi ndio maana vipaji vingi vipya havipenyezi. Tunaishia kuona vipaji vilevile.

Mwinyi Blog: Ni changamoto gani ulizokutana nazo toka uingie katika tasnia ya bongo movie?
Rachel Bithulo: Changamoto nilizokutana nazo wengi hawatambui thamani ya msani. Pia changamoto nyingine kubwa ni pesa ambapo unatumia mavazi kwa cost yako katika kufanikisha movie.

Mwinyi Blog: Wewe ni mrembo kiasi kwamba mwanaume yeyote rijali anaweza tamani kuwa nawe. Je, katika tasnia ya bongo movie unawezaje kuondokana na vishawishi vya wasanii wenzio kukutaka kimapenzi?
Rachel Bithulo: Naweza kukabiliana nao kwa kuwa na msimamo thabiti binafsi.

Mwinyi Blog: Je, kuna msanii yeyote aliwahi kukutumia kama video queen wa video ya wimbo wake? Maana najua wewe ni mwanamitindo unaweza kung'aa vyema katika video mbalimbali.
Rachel Bithulo: Msanii aliewahi ni PNC na video ya super nyota Dodoma aitwae Jaco Beats pia kuna mama Africa ya Bigbon90 kutoka Dodoma.

Mwinyi Blog: Unayatizamaje maisha yako baada ya miaka kumi ijayo ukijaliwa uhai?
Rachel Bithulo: Maisha yangu baada ya miaka kumi nategemea kuwa na familia pia nategemea kuwa mfanyabiashara mkubwa katika nyanda tofauti ikiwemo sanaa.

Mwinyi Blog: Je, huwa unafanya mazoezi ya mwili wako? 
Rachel Bithulo: Huwa najitahidi kufanya mazoezi ili nisizidi kunenepa zaidi.

Mwinyi Blog: Wasanii gani wa bongo movie unaowakubali kwa kazi zao?
Rachel Bithulo: Wasanii ninaowakubali ni Hajha Adam Haji, Irene Paul, Wolper, Single Mtambalike na Mboto Haji.

Mwinyi Blog: Ni movie gani ulizocheza ambazo zipo sokoni?
Rachel Bithulo: Movie ambazo nimecheza zipo sokoni ni October 3, Claritha na kidudumtu.

Mwinyi Blog: Asante sana kwa ushirikiano wako nakutakia kila la kheri katika kazi zako.
Rachel Bithulo: Asante kila la kheri na kwako pia.
Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.