Breaking News

Picha za Wema na Ommy Dimpoz Zawavutia Wengi Mtandaoni!



Siku ya juzi kwenye kurasa mbalimbali za watu maarufu kwenye mtandao wa INSTAGRAM walibandika picha hizi za mwanadada Wema Sepetu akiwa na Ommy Dimpoz wakiwa katika mapozi tofauti tofauti.
Kila zilipowekwa, wengi wa bonyeza kitufe cha kuzipenda na wengine waliandika maoni yao huku wengi wakiwasifia kwa jinsi walivyopendeza, na wengine walienda mbali zaidi kuwa wamependezana hivyo ingependeza hii iwe ni Le PROJECT mupyaaa.

Ila baadhi ya watu walibuka na kuponda bila sababu kibaya zaidi ni pale baadhi yao ambao sio waungwana na wamekosa maadili walikuwa wakiporomosha lugha za maji taka nakuleta mabishano ambayo huchafua kabisa “post” za watu.

Tujirekebishe jamani hata kama watu huwapendi sio vyema kutumia akaunti feki na kutukana watu kwa chuki zako binafsi. Hapa Wema na Ommy Dimpoz mmetokeleze, pokeeni LIKE!!
Mzee wa Ubuyu





Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.