Breaking News

P- FUNK AMTOA OFA GODZILLA




Mtayarishaji wa muziki na mwanzilishi wa Bongo Records, P-Funk Majani, ametoa ofa ya zaidi ya shilingi milioni 5 kwa Godzilla kumtaka warudie wimbo wake ‘Tungi’ uliopo kwenye mixtape yake, Zillax.







Godzilla amekiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM kuwa, mtayarishaji huyo mkongwe alisema yupo tayari kuurudia wimbo huo na kuufanyia video kutoka kwa director yoyote hapa nchini.

“Ni shabiki yangu pia ni producer, aliniambia yupo tayari kutoa dola elfu tatu turudie ile nyimbo tutoe na video atalipa,” alisema Zizi. “Ameniambia nichague director yoyote yeye yupo tayari kulipia dola elfu tatu au elfu nne kwa sababu ameupenda wimbo.”

“Anataka audio turudie na tumeshaongea na Nahreal na vocal tutafanyia kwake. Tulikutana kwenye sherehe moja ya Tuo8 January akaisikia ile nyimbo akadata, akasema nipo radhi kulipia dola elfu tatu ama elfu nne kulipia huu wimbo Nahreal arudie beat turekodi tena wimbo.”