Exclusive | Jifunze kuimba na Joett kupitia Mkito.com
Kwa mara ya kwanza kabisa, mtandao wa ku-download mziki
wakitanzania Mkito.com, unajiunga na mwalimu mahiri wa sauti Tony Joett,
kuwaletea watanzania huduma ya mafunzo ya sauti kwa wale ambao
wangependa kujifunza kuimba kupitia mtandao na kwa gharama nafuu,
nakupokea mafunzo yaliyo andaliwa kitaalamu kwa lugha ya Kiswahili na
ambayo yataweletea mafanikio ya haraka na ya uhakika.
Joett
ameandaa programu hizo za mafunzo ya sauti kwenye studio ya producer
Lucci wa Transformax Records, ambaye pamoja walikua majaji wa Airtel
Trace Music Star Season 2 mwaka 2016.
“Madhumuni ya kuandaa
mazoezi haya maalum,” alisema Joett “nikuwawezesha watanzania kujifunza
kuimba kwa urahisi, ili kutatua hili tatizo la vijana kuto jua
pakugeukia kupata mafunzo haya ya kitaalamu na ambayo yanakuza vipaji
kwa viwango vile vya kimataifa.”
Maandalizi ya
programu hizi yamegawanywa katika volume ama toleo 4, ambazo toleo la
kwanza ndio msingi; toleo la pili ni muendelezo; na toleo la 3 na la 4
zinaelekea kwenye viwango vya juu zaidi vya mafunzo ya kuimba, kwahivyo
ili kupata mafanikio mwanafunzi atahitaji kuanzia toleo la kwanza hadi
kufikia la 4 na kwa mpangilio huo maalum, alafu hatimaye kufanya mazoezi
yote manne kwa pamoja. Kwa ujumula, mazoezi yote manne kwa pamoja
yanachukua takriban dakika 30.
Vile vile kuna zoezi stahiki
la pumzi lililoandaliwa na Joett. Watu wanaopenda kujifunza kuimba
wataweza ku-download kila toleo kwa shilingi 250 tu, na kupata ushauri
na muongozo kutoka kwa Joett kupitia Mkito.com na blog ya
JoettMusic.com.
Joett ambaye pia hutoa mafunzo
ya sauti ya ana kwa ana katika studio yake jijini Dar es salaam, ni
mwalimu aliye bobea kwa kipindi kirefu na anao uzoefu na utaalamu katika
fani ya kufundisha sauti. Mafunzo anayotoa Joett yanasaidia kurekebisha
matumizi ya sauti ili kuondoa tatizo sugu la kuimbia kooni; kupiga
makelele wakati wakuimba; kuumia kooni na kukauka kwa sauti; na hujenga
uwezo wa sauti ya mwimbaji kwenda juu na kwenda chini kwa urahisi na
bila ya maumivu wala mateso ya aina yeyote. Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.