Kwa wale wapenzi wa BONGO MOVIE "CLARITHA" Coming Soon.
KinKwin Creative Production wanamtambulisha mrembo mwingine mwenye kipaji kwenye tasnia ya Bongo movie ajulikanae kwa jina la Rachel Njingo. Ambaye utapata kumuona katika filamu yao mpya "CLARITHA" ambayo ndani ya filamu hiyo amecheza pamoja na Mohammed Fungafunga a.k.a Jengua , Stanley Msungu na wengineo. Filamu hiyo inazungumzia mambo mengi ambayo utapata kuyajua pindi uionapo. Akiongea na Mwinyi Blog, Rachel Njingo amesema filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia weekend ya wiki ijayo. Hivyo wapenzi wote wa filamu wakae mkao wa kula maana chakula kitamu chenye viungo mbalimbali kimeishaiva.
Asante kwa kutembelea MWINYI BLOG naomba ubofye HAPA kuingia kwenye page yangu ya facebook na kulike page ili uendelee kupata burudani na matukio ya hapa na pale.