Breaking News

Kaa tayali kwa Ujio wa ANGEL BENARD



ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo.


Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.
 Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment. Stay connected with MWINYI BLOG.