Breaking News

Ujio mpya wa Nikki Mbishi, One The Incredible & Songa Feat. Lady Jay Dee - Kupanda na Kushuka


Wakitokea Tamaduni Music; Nikki Mbishi akiwa na One The Incredible pamoja na Songa wamemshirikisha Lady Jaydee katika kazi yao mpya 'Kupanda Na Kushuka' wanayotarajia kuiachia hivi karibuni.
Akiongelea kuhusu wimbo huo, Mbishi ameelezea sababu ya kuwashirikisha One Incredible, Songa pamoja na Jide kuwa ni kutaka kutengeneza muziki mzuri kwani wote kwenye wimbo huo wana ladha adimu hivyo wote kuwa katika kazi moja kutafanya wimbo uwe bora zaidi hivyo fans wategemee kitu kizuri kutoka kwao.


"Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani ili uwe mzuri zaidi na hii ni kawaida ya muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu kwa pamoja kitakuwa safi, tukaingia studio za Man Walter tukafanya wimbo 'Kupanda na Kushuka'. Ni wimbo ambao unaelezea maisha ya kawaida , kupanda na kushuka kwa maisha, leo umepata kesho umelala njaa lakini ni maisha...."
 
 
 Asante kwa kutembelea MWINYI BLOG naomba ubofye HAPA kuingia kwenye page yangu ya facebook na kulike page ili uendelee kupata burudani na matukio ya hapa na pale.