Breaking News

JAMAA MMOJA AANZISHA SHINDANO LA KUTAFUTA MABIKIRA NCHINI AFRIKA KUSINI, MSHINDI KUPATA R100,000




Una miaka 35 na bado ni bikira? Unaishi nchini Afrika Kusini? Jamaa mmoja aitwaye Rabelani Ramani [kwenye picha hapo juu] ameanzisha shindano au zoezi la kumpata wanawake au wasichana wenye umri wa miaka 35 na kuendelea ambao bado wamejitunza na hivyo kubakia bikira mpaka hivi sasa.



Jamaa huyo kutoka jimbo la Limpopo ambaye yeye mwenyewe ana umri wa miaka 29 na tayari ana watoto watano kutoka kwa wanawake wanne tofauti nje ya ndoa, anasema washindi watajipatia Randi 100,000 au chini ya hapo, medali za dhahabu,fedha na shaba kutegemea na umri.



Rabelani ambaye anaongoza shirika lisilokuwa na kiserikali lijulikanalo kama SA Virgin Girls Awards ambalo limesajiliwa kihalali anasema wazo hilo amelipata kama njia mojawapo ya kusaidia kujua hali halisi ya mimba zilizotarajiwa na maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa wanawake nchini Afrika Kusini.



Tayari taasisi yake imekusanya wafanyakazi wa kujitolea 31 ambao watasaidia kusambaza fomu mashuleni,sokoni, makanisani na kwingineko kwa yeyote anayetaka kushiriki. Tayari anao madaktari kadhaa ambao wamekubali kushirikiana naye katika zoezi la kupima ubikira.
 
 Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale