Breaking News

WAKAZI NDANI YA MKASI LEO


WAKAZI, mmoja wa manguli wa Muziki wa Hip Hop Tanzania, sio tu ametokea kufana ndani, lakini pia amepata nafasi za kuonyesha umahiri nje ya mipaka yetu! Jina halisi Webiro Wasira, mashabiki wake hupenda kumuita “Beberu” na yeye hupenda kujifananisha na “The Beast” (Mnyama)!
Toka Kwa Obama ambapo alifanya kazi zake nyingi za awali, hadi kurudi nyumbani na kuendeleza fani, na hatimae kupata nafasi kufanya onesho katika jukwaa la kimataifa ikiwemo katika Moja ya “Eviction Shows” za Big Brother Africa huko Afrika Kusini. 

Kama ilivo kwa wasanii wengi, safari yao sio rahisi, na kufika kivulini bado mwendo mrefu….je yeye Wakazi ana lipi la kusema? Ungana nasi leo Saa 3:30 usiku, kwani Mkasi TV watakaa ana kwa ana na The Beast atueleze kinaugaubaga! Yote ni kupitia Chaneli yako ya EATV kwa hisani kubwa ya Tusker Lager (TZ), Airtel Tanzania na Coca Cola. Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.