Breaking News

[Story] Mjue Movie Star “Angelina Jolie – Pitt”



Ukizungumzia mastaa wakubwa wengi wanaotingisha Hollywood kwa majina makubwa ambayo yametikisa dunia ya FILAMU huwezi muacha mrembo huyu ajulikanae kwa jina la Angelina Jolie, Angelina Jolie ni mzaliwa wa mnamo mwaka 1975 tarehe 4 july huko Los Angeles California actress. Licha ya kuwa na watoto 6 kati aliozaa mwenyewe na adopted ambao aliamua kuwachukua Afrika na Asia na kuwapa apportunity ya Maisha, Angelina Jolie ameweza kuwa Mama na ameweza kuendelea kufanya kazi zake na pia kubaki kuwa mrembo ambae anazungumziwa mpaka leo.

Urembo wake umedhihirishwa kwa yeye kushinda tuzo kadha wa kadha kwenye urembo kama “Sexiest Celebrity” mnamo mwaka 2006 alitangazwa na E! channel. Vile vile ni moja kati ya watu ambao wanatazamwa kama kioo cha Jamii Dunia (World influential People) kutokana na uigizaji wake machachari na kuwa “Humanitarian Ambassador” wa United Nations.

Actress huyu aliapata nafasi ya kuonekana duniani kupitia filamu yake yake ya Tomb Raider (2001) ikifatiwa na part ya pili kazi hizi zilimpa jina jina kubwa na umashuhuri mkubwa. Mnamo mwaka 2010 alipotoa Salt alitingisha dunia na kujizolea pesa kibao $20,000,000. Na Filamu nyingine nyingi kama Mr & Mrs Smith ambayo ilimfanya aweze kutengeneza mahusiano na Star mwingine wa Filamu ajulikanaye kama BRAD Pitt ambae ndio mume na baba wa watoto wake.

Licha ya kuwa muigizaji mzuri , wakati wa udogo wake alitarajia kuwa funeral director na sio muigizaji. Angelina Jolie ameshaudhihiriahia ulimwengu kuwa na kipaji kwa kupokea tuzo kadhaa kama OSCARS kwenye Filamu “Girls Interrupted” (Best Supporting Actress – 2000), Silver Berlin Bear 2007, MTV Movie Awards 2010 na Humanitarian Awards 2014.

Hollywood star huyu hivi sasa tunatarajia kupokea kazi yake nyingine ambayo inaitwa ”Maleficient”. Katika filamu hii ameshirikiana na mastaa wengine kama Elle Fanning, Sharlto Copley, Miranda Richardson na filamu hii imetokana na story ya watoto ijulikanayo kama ”Sleeping Beauty” filamu hii inatarajiwa kutoka May 30, 2014.

Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.