Breaking News

Basi la Bunda Express lagongana na Treni Manyoni mkoani SingidaMtu mmoja amefariki dunia na wengine 38 wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya basi la Bunda Express walilokuwa wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza kugongana na Treni eneo la Manyoni Mkoani Singida. Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi hii limegongana na Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukio kinasema kuwa watu wanne wamefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa. Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

4 comments: