.

.
PATA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA PANDE TOFAUTI TOFAUTI NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UNAWEZA KUTANGAZA NAMI TUKIO LAKO MUHIMU KAMA SHEREHE ZA HARUSI, HAPPY BIRTHDAY, GRADUATION NA NYINGINEZO KWA BEI POA. WASILIANA NAMI KUPITIA 0754667930 AU 0653599393. NYOTE MNAKARIBISHWA.

Saturday, March 9, 2013

CORD kupinga matokeo ya urais makahamani
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga

Muungano wa CORD wake Raila Odinga umeelezea kuwa unajianda kwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta

Raila Odinga, ameambia waandishi wa habari kuwa kuwa matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalikuwa yamehujumiwa hasa baada ya kutokea hitilafu katika mitambo ya elektroniki iliyokuwa inatumiwa katika shughuli hiyo.

Raila amedokeza kuwa muungano wao unajiandaa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Aidha alisema kugoma kwa mitambo hiyo kulichanganya mambo katika shughuli ya kuhesabu kura. Alisema kuwa baada ya kutokea hitilafu, kura alizokuwa amepata katika maeneo bunge ambayo ni ngome zake , ziliongezwa kwa hesabu ya kura za muungano pinzani wa Jubilee.

Mapema wiki hii, wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais ilikuwa inafanyika, CORD walielezea malalamishi kuhusu shughuli nzima hasa baada ya kura kuanza kuhesabiwa kwa mikono badala ya mashine.

Lakini mahakama kuu ilitupilia mbali kesi yao ikisema kuwa haina uwezo wa kufanya uamuzi katika kesi hiyo, na kuwa ni mahakama ya juu zaidi pakee inayoweza kusikiliza kesi hiyo.CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

.