Breaking News

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA PILAU YA MBOGA MAJANI



KAA TAYARI KABISA KWA KUJIFUNZA KUPIKA PIALU HII YA MBOGA MAJANI

MAHITAJI
250 gram mchele wa basmati 1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds) 1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala 1/2kijiko kidogo cha chai coriander powder 1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder 60 gram njegere za kuchemshwa 1 kitunguu maji chop chop 3 nyanya za kuiva nazo chop chop 1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa 1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa 2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo 60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima) 1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha

JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15 Muda wa mapishi : Dakika 30 Idadi ya walaji : Watu 2

 

Kwenye kikaango weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kama ni samli au siagi, kisha graham masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande vidogo kama inavyoonekana kweny picha. Kisha weka chumvi, karafuu na pili pili manga endelea kukaanga.




UKisha pata harufu ya kunukia saafi imeenea jiko zima hahahahaaaa !! na mboga zako ziwe zimeanza kuiva na hazijaregea basi anza kumimina mchele kidogo.




Endelea kukaanga wali wako na ukiuchanganya uchanganyike vizuri kabisa na mboga kwa dakika 2 au 3inategemea na moto wa jiko lako au ubora wa sufuria yako.




Kisha weka gram 600 za maji ni sawa na nusu lita na 100 gram za maji kisha koroga na funika na mfuniko acha iive kwa dakika 10 kwa moto wa wastani.




Baada ya dakika 10 itakua imekaribia kabisa kuiva, kisha weka njegere za kuiva na koroga kidogo ichanganyike kisha pika kwa dakika 2 tena.



Baada ya pilau yako kuiva basi juu yake rushia majani ya mint au giligilani kuongeza uzuri wa rangi, ladha na harufu safi sana katika pilau yako.



Mwisho kabisa pia ukiwa mpenzi wa siagi mwagia kwajuu kiasi au unaweza mwagia samli hii nikuongeza harufu nzuri na ladha zaidi.




Usisahau kwajuu kabisa mwagia karanga au korosho za kukaangwa.  Kumbuka kuaandaa mchuzi mzito kabisa pembeni kwajili ya kulia chakula chako. Kwamapishi haya haya unaweza pika ikawa pilau ya nyama ya kuku, mbuzi au ng'ombe kumbuka kuikata kata nyama na unaiweka mwanzo kabisa wakati unakaanga viungo itaiava sambamba na wali wako na itapendeza sana.

No comments